Na Samwel Mtuwa, Dodoma
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki leo amekutana na balozi wa Japani nchini, Masaharu Yoshida
mjini Dodoma lengo likiwa ni kujadiliana
namna ya kushirikiana kwenye uwekezaji wa madini nchini.
Akizungumza katika
kikao hicho, Waziri Kairuki alisema lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili
maandalizi ya Jukwaa la Uwekezaji katika
Sekta ya Madini kati ya Tanzania na Japan.
Alisema kupitia jukwa
hilo, wadau kutoka nchi zote mbili watafahamu
fursa za uwekezaji katika sekta
ya madini kama vile uongezaji thamani ya
madini yapatikanayo nchini na namna ya kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo.
Kairuki aliongeza
kuwa mbali na fursa mbalimbali katika sekta ya madini jukwaa hilo litaangalia
namna ya kuongeza ajira kwenye sekta hiyo kwa kuwajengea uwezo wadau wa madini
nchini.
Balozi Yoshida aliambatana
na Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya uwekezaji
katika sekta ya madini.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida (kulia) ofisini kwake mjini Dodoma mapema leo tarehe 09 Mei, 2018. |
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akiagana na Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida (kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho. |
No comments:
Post a Comment