Na Greyson Mwase,
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 06 Mei, 2018 amekutana na wachimbaji
wa madini ya ujenzi aina ya kokoto katika eneo la Lugoba wilayani Bagamoyo
mkoani Pwani. Mkutano huo uliohusisha Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mbunge wa
Chalinze, Ridhiwani Kikwete na wananchi, ulilenga kujadili changamoto katika
uchimbaji madini ya ujenzi aina ya kokoto.
Katika mkutano huo, Naibu Waziri Biteko alitoa
maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na wawekezaji kuendeleza maeneo yao, wawekezaji kutouza leseni kwa mtu mwingine
pasipo kushirikisha serikali, wawekezaji kuandaa mpango wa utoaji huduma
kwa jamii pamoja na kuutekeleza na Ofisi
ya Madini ya Kanda ya Mashariki kufuatilia ahadi za wawekezaji katika huduma za
jamii na kuwasilisha ripoti mara moja.
Maelekezo
mengine ni pamoja na Ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki kuwasilisha ripoti ya athari za mazingira kabla ya Mei
20, 2018, wawekezaji kushirikiana na wananchi wanaowazunguka, kampuni zenye
mgogoro na wananchi kuhakikisha zinamaliza tofauti zao na fedha za
halmashauri kutumika kwenye uwekezaji
mwingine kwa ajili ya maendeleo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wananchi mbalimbali walioshiriki katika mkutano huo. |
Sehemu
ya wakazi wa eneo la Lugoba lililopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa
unatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani).
|
Mchimbaji
kutoka kampuni ya Gulf Concrete and Cement Products, Augustine Modest
akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani)
katika mkutano huo.
|
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko akinukuu maswali mbalimbali yaliyokuwa yanaulizwa
na wachimbaji madini ya kokoto (hawapo pichani) katika mkutano huo.
|
No comments:
Post a Comment