Na Mohamed Saif,
Wataalam
wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wamekutana
Jijini Arusha ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu madini hayo kwa
maslahi mapana ya nchi hizo.
Mkutano
huo wa siku mbili ulifunguliwa jana Machi 27, 2018 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo ambapo alisisitiza kuwa Nchi Wanachama wa ICGLR wanao wajibu wa
pamoja kuhakikisha malengo waliyojiwekea yanafikiwa kwa manufaa ya wanachama
wote.
Gambo
alizungumzia changamoto mbalimbali zinazozikabili Nchi Wanachama ambazo ni
uvunaji haramu wa madini, utoroshwaji wa madini, uharibifu wa mazingira,
ukosefu wa teknolojia na baadhi ya Nchi kuwa na changamoto za Kiusalama.
Hata
hivyo alisema changamoto hizo zisiwe sababu ya kurudi nyuma badala yake juhudi
za pamoja, mshikamano wa dhati unahitajika ili kukabiliana na changamoto hizo
na kuhakikisha ufumbuzi unapatikana kwa maslahi mapana ya Nchi za Ukanda wa
Maziwa Makuu.
Nchi
Wanachama ni Tanzania, Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo
(Kinshasa), Congo (Brazzaville), Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan Kaskazini,
Uganda na Zambia.
Tanzania
imekuwa Mwanachama rasmi wa ICGLR Mwaka 2008 na tangu wakati huo imeendelea
kutekeleza malengo ya mpango wa ICGLR ili kufanikisha udhibiti wa uvunaji
haramu wa madini na kuhakikisha manufaa ya pamoja ya rasilimali husika
yanapatikana.
Wataalam
wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na
majadiliano.
|
Baadhi
ya Washiriki wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda
wa Maziwa Makuu ICGLR wakifuatilia majadiliano
|
Mwenyekiti
wa mkutano, Service Julie kutoka Congo (wa pili kulia) akizungumza wakati wa Mkutano
wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR.
|
Wataalam
wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na
majadiliano Jijini Arusha.
|
No comments:
Post a Comment