Na Asteria Muhozya, Mirerani
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko amesema Ujenzi
wa Ukuta kuzunguka Migodi ya Mirerani ni jambo la Kihistoria na kwamba
linatarajiwa kuweka rekodi Barani Afrika.
Naibu Waziri Biteko aliyasema hayo
tarehe 23 Machi, wakati wa kikao cha Maandalizi ya Uzinduzi wa Ukuta huo
unaotarajiwa kuzinduliwa mapema mwezi Aprili na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Magufuli.
Aliongeza kuwa, ukuta huo ni jambo
ambalo watanzania wamelisubiri kwa miaka mingi licha ya kuwepo kwa mapendekezo
na sasa hatua zimechukuliwa na kutekelezwa.
Pia alilipongeza Jeshi kwa nidhamu
kubwa ambayo limeonesha kwa ujenzi wa ukuta huo wenye urefu wa kilomita
25.4 na ambao ujenzi wake umechukua kipindi cha miezi 3 tofauti na
ilivyopangwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, Alexander Mnyeti, alilipongeza Jeshi kwa kazi ambayo imefanyika na
kuwataka Wajumbe wa Kamati kukamilisha utekelezaji wa majukumu yote kwa
wakati.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa
Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa
Wilaya ya Simanjiro Zephania Chaula, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Manyara na Wilaya ya Simanjiro, Wizara ya Madini, Wizara ya Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) , Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO - Manyara) na Wakala
wa Barabara ( TANROAD)
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kulia),
akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Manyara Alexander Mnyeti mara baada ya
kikao cha Maandalizi ya Uzinduzi wa Ukuta wa Mirerani.
|
Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimaliwatu Issa Nchasi, (wa pili
kulia) wakibadilishana jambo na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi wa Ukuta wa Mirerani.
|
Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimaliwatu Issa Nchasi akimweleza
jambo Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko mara baada ya kikao cha maandalizi.
|
Baadhi ya Wajumbe wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Manyara na Wilaya ya Simanjiro
wakibalishana jambo.
|
No comments:
Post a Comment