Na Asteria Muhozya,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini , Profesa Simon Msanjila leo tarehe 18 Machi, amekutana na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Uzinduzi wa Ukuta unaozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite Mirerani, Wilayani Simanjiro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini , Profesa Simon Msanjila leo tarehe 18 Machi, amekutana na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Uzinduzi wa Ukuta unaozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite Mirerani, Wilayani Simanjiro.
Ukuta huo unatarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli mapema mwezi Aprili.
Kikao hicho kimewashirikisha Watumishi kutoka Wizara ya Madini,
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Makamanda kutoka Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Akizungumza katika kikao hicho Prof. Msanjila amelipongeza Jeshi
kwa ujenzi wa kasi wa ukuta huo na kuongeza kuwa ilikuwa ni kazi ya
kujitolea na jeshi limeisimamia vizuri.
Kwa upande wake, Naibu Kamanda wa Oparesheni ya ujenzi wa ukuta
huo, Luteni Kanali Rashidi Kanole amesema kuwa, siri ya ujenzi wa ukuta
kuchukua muda mfupi tofauti na muda wa utekelezaji wake, pamoja na mambo
mengine umetokana na kufanya kazi kwa kuzingatia utamaduni wa jeshi unaohusisha
kiapo na uzalendo na kutafuta mbinu za changamoto bila kusubiri viongozi wa juu
kwenda kutatua changamoto hizo.
Ujenzi wa ukuta huo ulipangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi
sita lakini umekamilika ndani ya kipindi cha miezi 3.
Sambamba na kikao hicho, pia, Prof. Msanjila amekutana na
wadau wa madini wilayani humo kujadili masuala mbalimbali kuhusu biashara
ya madini hayo mara baada ya ukuta wa kuzinduliwa.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na ulinzi shirikishi wa
ukuta huo, biashara ya Tanzanite, uwazi wa biashara na suala la vitambulisho
vya Taifa.
Kuhusu vitambulisho Prof. Msanjila amesema kuwa atakayeingia
ndani ya ukuta huo ni yule tu atakayekuwa na kitambulisho cha Taifa.
Aidha, pande zote mbili Serikali na wadau wamekulllliana
kukutana tena illlmujadili kwa kina suala la biashara ya madini hayo mara
baada ya ukuta kuzinduliwa.
No comments:
Post a Comment