Na Mohamed Saif
Wananchi
wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo Wilayani
Shinyanga wametakiwa kufanya subira wakati mgogoro wao wa fidia na mwekezaji
ambaye ni Kampuni ya uchimbaji madini ya Henan Afro Asian Engineering
ukitafutiwa ufumbuzi.
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa wito huo Machi 12, 2018 kwenye mkutano na
wananchi hao uliofanyikia kwenye Kitongoji cha Mahiga na kuhudhuriwa na
watendaji mbalimbali wa Serikali.
Mkutano
huo unafuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Magufuli alilolitoa Machi 11, 2018 kwenye mkutano na wananchi wa Kahama ambapo
alielezwa na Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum kuwa wananchi wa Mahiga wana
mgogoro wa muda mrefu na mwekezaji hususan kuhusiana na suala la ulipaji fidia
ili kupisha mradi.
Kufuatia
maelezo hayo ya Mbunge, Rais Dkt. Magufuli alimuagiza Naibu Waziri Biteko
kuhakikisha anafika kwenye eneo hilo ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza
wananchi.
Rais
Magufuli alisisitiza kuwa ni wakati sasa Watanzania waanze kunufaika na
rasilimali zao ikiwemo madini. "Tunataka madini yawanufaishe
Watanzania," alisema Rais Magufuli.
Alisema
wawekezaji wakifika nchini ni lazima wahakikishe Watanzania wananufaika kwa
namna mbalimbali ikiwemo ajira, kodi na tozo.
"Jukumu
langu nimeamua kusimamia suala hili; Nawahakikishia Serikali iko imara kwa
ajili ya kuwatetea wanyonge," alisema Rais Dkt. Magufuli.
Aliagiza
mwekezaji atakayehitaji kuchimba kwenye maeneo yenye wachimbaji wadogo ni
lazima kwanza akubaliane nao ikiwemo suala la ulipaji wa fidia na sio
kuwafukuza.
"Suala
la wachimbaji lizingatiwe kwa mujibu wa sheria. Tuwalee ndio maana tumeanzisha
vituo vya mfano maeneo mbalimbali ili wajifunze," alisema.
Aidha, kwa
mujibu wa Mbunge huyo ni kwamba mgogoro huo ulianza tangu Julai 2017 baada ya
mwekezaji huyo kuanza shughuli zake za kuandaa mazingira ya kuchimba bila kuwa
na makubaliano maalum na wananchi hao.
Akiwa
katika mkutano na wananchi hao, Biteko alielezwa kero mbalimbali zinazowakabili
ikiwemo kutoridhishwa na kiasi cha fidia kilicholipwa ili kupisha maeneo yao
kwa ajili ya mwekezaji, wengine kutohitaji kabisa fidia na maombi ya baadhi yao
kuruhusiwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na uchimbaji kwenye
maeneo husika.
Biteko
aliwataka kufanya subira wakati Serikali inatazama namna bora ya utatuzi wa
hoja zao kwa mujibu wa sheria ili manufaa yapatikane bila kumuonea yoyote.
Alisema
Rais Dkt. John Magufuli anataka kuona Watanzania wanyonge wananufaika na
rasilimali zao ikiwemo rasilimali madini.
“Serikali
ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ni Serikali
inayowaangalia wanyonge. Nimesikiliza kero zenu nitazifikisha na hatua
itachukuliwa kwa mujibu wa sheria. Mfanye subira," alisema Biteko
Aliongeza
kuwa Serikali haipo tayari kuona Watanzania wanyonge wanateseka na kwamba
wakati umefika wa wao kunufaika.
Alifafanua
kuwa suala lao litashughulikiwa kwa wakati na kwa kuzingatia Sheria ili haki
itendeke pasipo kumuumiza yoyote.
Hata hivyo
aliwakumbusha wananchi hao kuhakikisha wanafuata utaratibu na sheria ili
manufaa yapatikane bila kuleta madhara yoyote.
Aidha, kwa
mujibu wa Mthamini wa Wilaya ya Shinyanga, Devotha Njella ni kwamba wananchi
waliofanyiwa tathmini ni 500 na kwamba bado mwananchi mmoja mwenye heka 25 na
nyumba 6 ambaye alikataa.
Alifafanua
kwamba malipo hayo ya fidia yalifanyika kwa awamu mbili na kwamba katika awamu
ya kwanza Shilingi 953,194,050.75 zililipwa na awamu ya pili kiasi kilicholipwa
ni Shilingi 472,413,686.32 na kwamba bado kiasi cha Shilingi 208,886,951.01
ambacho taratibu za kulipa zinaendelea.
Wananchi wa
Kijiji cha Mwakitolyo, Wilayani Shinyanga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini,
Doto Biteko (hayupo pichani) akizungumza kuhusu mgogoro wao na Kampuni ya
uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.
|
Mbunge wa
Jimbo la Solwa, Ahmed Salum akizungumza na wananchi wake wa Kitongoji cha
Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo Wilayani Shinyanga kuhusiana na
mgogoro wao na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro
Asian Engineering.
|
Mkuu wa Wilaya Shinyanga
Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa Mwakitolyo, Wilayani Shinyanga wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa
Madini, Doto Biteko (hauypo pichani).
|
Naibu Waziri
wa Madini, Doto Biteko (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum
(anayemfuatia) wakisikiliza kero za wananchi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji
cha Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo Wilayani Shinyanga kuhusiana na mgogoro wao na
mwekezaji ambaye ni Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian
Engineering.
|
No comments:
Post a Comment