Monday, March 5, 2018

Naibu Waziri Nyongo atembelea ofisi ya Madini Kigoma


Na Veronica Simba, Kigoma

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ametembelea Ofisi ya Madini Kigoma na kuzungumza na wafanyakazi, akiwa katika ziara ya kazi mkoani humo, Machi 3 mwaka huu.

Katika kikao hicho, wafanyakazi walipata fursa ya kujadiliana na Naibu Waziri kuhusu utendaji kazi katika eneo lao, yakiwemo mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo.

Naibu Waziri aliwapongeza wafanyakazi hao kwa utendaji kazi mzuri na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto walizowasilisha, ikiwemo upungufu wa watumishi.

Hata hivyo, aliwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili kuhakikisha wanakusanya maduhuli ya Serikali kwa kiwango kinachotakiwa ili Sekta hiyo iweze kukuza mchango wake katika Pato la Taifa.


Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini Kigoma alipowatembelea na Kuzungumza nao, akiwa katika ziara ya kazi mkoani humo, Machi 3 Mwaka huu.


Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini Kigoma alipowatembelea na Kuzungumza nao, akiwa katika ziara ya kazi mkoani humo, Machi 3 Mwaka huu.


Mjiolojia katika Ofisi ya Madini Kigoma, Laurent Bujashi (kushoto) akimwonesha Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (katikati) aina za Madini yanayopatikana mkoani humo, wakati Naibu Waziri alipotembelea Ofisi hiyo na kuzungumza na wafanyakazi, akiwa katika ziara ya kazi Machi 3 Mwaka huu.


Muhudumu katika Ofisi ya Madini Kigoma, Laulencia Masabo akizungumza wakati Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), alipotembelea Ofisi hiyo na Kuzungumza na wafanyakazi, akiwa katika ziara ya kazi mkoani humo, Machi 3 Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment