Na
Mohamed Saif,
Naibu Waziri wa Madini,
Doto Biteko amezikumbusha Kampuni za Madini nchini kuhakikisha suala la
mahusiano na jamii linapewa kipaumbele ili kuboresha utendaji wa shughuli zao.
Amesema hayo Machi 5,
2018 Mkoani Geita alipokutana na wawakilishi wa Kampuni ya OreCorp Tanzania
Limited yenye Leseni ya Utafiti ambayo inatarajia kuanzisha shughuli za
uchimbaji mkubwa wa dhahabu kwenye eneo la Nyanzaga, Wilayani Sengerema.
Katika mkutano huo
uliofanyikia kwenye Ofisi za Madini, masuala mbalimbali ya shughuli za
uchimbaji madini yalijadiliwa na msisitizo ukiwa kuhakikisha suala la
uboreshaji wa mahusiano na jamii zinazozunguka miradi linapewa kipaumbele.
Biteko alisema uboreshaji
wa mahusiano na jamii ni kwa faida ya kampuni kwani kufanya hivyo kutasaidia
kuepuka migogoro isiyo ya lazima na hivyo kuboresha utendaji kazi na kuwa na
uzalishaji wenye tija.
Aidha, awali kabla ya
kukutana na kampuni hiyo, Biteko alikutana na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda
ya Ziwa Viktoria Magharibi, Mhandisi Yahya Samamba na Afisa Madini Mkoa wa
Geita, Mhandisi Ally Maganga.
Naibu Waziri Biteko
atahitimisha ziara yake hapo baadaye leo hii Machi 6, 2018 kwa kutembelea
machimbo ya dhahabu ya Nyang'wale na kuzungumza na wachimbaji kwenye machimbo
hayo.
Naibu Waziri wa Madini,
Doto Biteko akizungumza wakati wa kikao na wawakilishi wa Kampuni ya OreCorp
Tanzania Limited (hawapo pichani) walipokutana kwenye Ofisi za Afisa Madini
Mkoa wa Geita.
|
Naibu Waziri wa Madini,
Doto Biteko (mbele katikati) akizungumza na wawakilishi wa Kampuni ya Ore Corp
Tanzania Ltd.
|
Naibu Waziri wa Madini,
Doto Biteko (katikati) akijadiliana jambo na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda
ya Ziwa Viktoria Magharibi, Mhandisi Yahya Samamba (kulia). Kushoto ni Afisa
Madini Mkoa wa Geita Mhandisi Ally Maganga.
|
No comments:
Post a Comment