Na
Veronica Simba, Dodoma
Wafanyakazi wa Wizara
za Nishati na Madini walioko Makao Makuu mjini Dodoma, leo Machi 8 wameshiriki
maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Sherehe za
Maadhimisho hayo zimefanyika ki-Mkoa katika Eneo la Msalato na kushirikisha
Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, Mashirika Binafsi na baadhi ya
wanafunzi wa Shule mbalimbali.
Kaulimbiu ya
Maadhimisho ya Sherehe hiyo Kitaifa, kwa Mwaka huu ni ‘Kuelekea Uchumi wa
Viwanda, Tuimarishe Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini’.
Pichani ni matukio
mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment