Monday, February 26, 2018

Ziara ya Naibu Waziri Nyongo Geita


Na Veronica Simba, Geita

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amefanya ziara ya kazi Mkoa wa Geita, ambapo ametembela maeneo mbalimbali zinakofanywa shughuli za madini, pamoja na kuzungumza na wananchi.

Ujumbe mkuu alioutoa katika ziara hiyo ni kwa wote wanaojishughulisha na kazi za madini kuhakikisha wanakuwa na leseni halali, ili watambuliwe na Serikali, walipe kodi na tozo zote stahiki, ili mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa uongezeke.

Pia, ujumbe mwingine mkuu alioutoa ni kwa wadau wote wa sekta hiyo kushirikiana na Serikali katika zoezi linaloendelea la kuwabainisha na kuwafichua wote wanaoshiriki kutorosha madini.

Naibu Waziri alitembelea Mgodi wa Dhahabu wa Geita, Kijiji cha Nyakabale, Mtaa wa Nyamalembo pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Maeneo mengine ni katika Migodi ya wachimbaji wadogo wa madini ya Nsangano, Ahmed Mubarak, Busolwa, eneo la Mgodi unaomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ambako wachimbaji wadogo wanaendelea na uchimbaji, pamoja na eneo la uchenjuaji madini lililopo Nyarugusu.

Picha zifuatazo zinaonesha matukio mbalimbali wakati wa ziara hiyo.






No comments:

Post a Comment