Na Zuena Msuya, Shinyanga
Serikali
imetoa mwezi mmoja kwa Kampuni ya Uchimbaji madini ya Almasi ya El Hilal kulipa
zaidi ya Shilingi bilioni 3.4 ikiwa ni ada ya mwaka pamoja na mrabaha wa mauzo
ya almasi nchini na endapo itashindwa kufanya hivyo itafutiwa leseni yake.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kukagua migodi
ya
uzalishaji almas ya kampuni za Wiliamson Diamond na El Hilal
zilizopo
eneo la Mwadui mkoani Shinyanga,Februari 21, 2018.
Prof.
Msanjila alisema mgodi wa El Hilal unamiliki leseni
kubwa
ya uchimbaji wa madini ya almas,iliyotolewa mwaka 2010 na unadaiwa ada ya mwaka
( annual rent) Dola za Kimarekani 1,447,360 sawa na shilingi bilioni 3.1 ambazo
hazijalipwa kwa kipindi cha miaka 6, kuanzia 2012/13 hadi 2017/18.
Vilevile
aliweka wazi kuwa kampuni hiyo pia inadaiwa zaidi ya kiasi cha shilingi milioni
294.2 ikiwa ni mrabaha pamoja na adhabu yake iliyotokana na mauzo ya ndani ya
almasi yaliyofanyika
kwa
kipindi cha miaka tatu kuanzia 2011 hadi 2013.
“
Haiwezekani kampuni ikawa inafanya biashara ndani ya kipindi
chote
hicho halafu hailipi mapato ya Serikali, Sheria ya madini ya mwaka 2010
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 iko wazi inaelekeza hatua za kuchukua kwa
vitendo kama hivyo, sasa tumewapa muda na sheriaitachukua mkondo wake”, alisema
Msanjila.
Aidha
aliitaka kampuni hiyo kufanya shughuli zake kwa kuziangatia Sheria na Kanuni za
uchimbaji madini, na pia
katika
kutoa ajira kwa wafanyakazi wake na kwamba sheria na kanuni za madini zinapaswa
kufuatwa hata kama
ni
mwekezaji mzawa.
Sambamba
na hilo,Msanjila ilizitaka kampuni za uchimbaji zinazoendeshwa na wawekezaji wa
nje kuwa na akaunti
za
fedha hapa nchini tofauti na ilivyo sasa ambapo kampuni nyingi akaunti zake
zipo nje ya Tanzania.
Msanjila
pia aliwataka Makamishna Wasaidizi wa Madini kote nchini kufanya kazi kwa
kuzingatia weledi, juhudi na maarifa na bila kumpendelea mtu yeyote wakati
wakitekeleza
majukumu
yao.
Vilevile
aliwataka kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali katika
madini yanayopatikana kwenye maeneo yao, akitolea mfano wa Madini ya Ujenzi kuwa
yamesahaulika kabisa katika makusanyo.
Aliendelea
kuwakumbusha Makamishna hao kuendelea kutoa
elimu
sahihi kwa wachimbaji na wadau wote wa madini katika maeneo yao juu ya
marekebisho ya Sheria ya Madini ya
mwaka 2017 pamoja
na kanuni zake.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon
Msanjila,( wa tatu kushoto) akionywesha baadhi ya mitambo ya Mgodi wa uchimbaji almasi ya El Hilal iliyopo Mwadui, Shinyanga.
|
Katibu Mkuu
Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila,( wa pili kushoto)akikagua eneo ambalo
linatumiwa na Mgodi wa El Hilal kuchimba Madini ya Almasi.
|
Katibu Mkuu
Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila,( wa pili kushoto(
katikati)akionyeshwa sehemu ya mitambo ya Mgodi wa El Hilal unaochimba Madini ya
Almasi.
|
No comments:
Post a Comment