Na Mwandidhi Wetu Misungwi
Akiwa
katika ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wilayani humo, Nyongo alisema kuwa mwekezaji huyo alipewa
leseni ya uchimbaji wa madini kwa kipindi cha miaka 10 na hakuna uendelezaji
wowote alioufanya katika machimbo hayo.
Uamuzi
huo umetokana na malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho wakati wakitoa dukuduku zao kwa Waziri Mkuu
kuwa, mwekezaji huyo amekuwa akiwazuia wachimbaji
wadogo kuchimba madini katika machimbo hayo hali iliyopelekea Waziri Mkuu kumtaka
Naibu Waziri wa Madini kulitolea ufafanuzi suala hilo.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu mwekezaji huyo, Nyongo
alisema kuwa kutokana na kutoendeleza machimbo hayo mwekezaji huyo
amekuwa haelewani na jamii inayozunguka
machimbo hayo na kwamba hapo awali
wananchi walikuwa wanafanya shughuli za
uchimbaji katika katika eneo hilo
kabla ya kupewa mwekezaji huyo.
‘’Mwekezaji
huyu anayefahamika kwa jina la Badir Soud kwa kuwa leseni yake imeisha na
ameomba tena leseni hiyo ya uchimbaji hatutampa, na sisi kama Wizara ya Madini
tutawapatia wananchi wachimbe wakiwa katika mfumo wa vikundi’’ alisema Nyongo.
Aliendelea kueleza kuwa, pamoja na kutokuendeleza mgodi huo katika
kipindi hicho, mwekezaji huyo hajapeleka
vifaa kwa ajili ya shughuli za uchimbaji katika eneo la mgodi jambo ambalo
linaikosesha Serikali mapato.
Naibu
Waziri Nyongo alitumia fursa hiyo kuwaagiza wachimbaji wa madini nchini kufanya
kazi kwa mujibu wa Sheria za uchimbaji
madini ili waweze kutambulika rasmi na kuweza
kulipa kodi serikalini.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo |
No comments:
Post a Comment