Na
Mohamed Saif
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameupa Siku 14
Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi uliopo Mkoani Katavi kuhakikisha uwe
umepunguza wafanyakazi wa kigeni na kuajiri Watanzania kwenye nafasi wanazomudu
kama Sheria inavyoelekeza.
Alitoa agizo hili jana Tarehe 24 Februari, 2018
alipofanya ziara kwenya mgodi huo ili kujionea shughuli zinazofanyika katika
mgodi huo.
Taarifa ya mgodi iliyowasilishwa kwake ilibainisha
kuwa jumla ya wageni 48 wameajiriwa na huku 36 kati yao wakiwa hawana ujuzi na
wanafanya shughuli ambazo Watanzania wanamudu, ikiwemo ya ulinzi.
Biteko alisema dhamira ya Serikali ni kuona
Watanzania wananufaika na Sekta ya Madini kwa namna mbalimbali ikiwemo ya
kujipatia ajira kwenye migodi na kwamba suala hilo la kuajiri wageni kwenye
nafasi wanazomudu Watanzania halivumiliki.
Alimuagiza Mkuu wa Wilaya na Afisa Madini
kuhakikisha wanalifuatilia jambo hilo na liwe limemalizika baada ya wiki mbili
kuanzia Tarehe 24 Februari, 2018 na apatiwe mrejesho wake.
“Mnawafanyakazi wengi ambao wanafanya kazi ambazo
Watanzania wanaziweza. Hatuwabagui lakini tunataka manufaa ya madini yabaki kwa
Watanzania,” alisema Biteko.
Biteko aliiagiza Idara ya Uhamiaji Nchini
kufuatilia Wafanyakazi wakigeni waliopo migodini ili kukagua kama wanavyo
vibali vya kufanya kazi hapa nchini. “Mnavyotoa vibali muwe makini, ili
shughuli zinazokuja kufanywa na wageni ziwe kweli Watanzania hawazimudu,”
alisisitiza.
Alihimiza migodi yote nchini kuepuka kuwanyanyasa
wafanyakazi sambamba na kuwataka wafanyakazi waliaoajiriwa migodini kufanya
kazi kwa uaminifu ili kulijengea Taifa heshima inayokubalika.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia)
akisalimiana na Wafanyakazi wa Kigeni (Wataalam wa Nje/expatriates) wa Mgodi wa
Dhahabu wa Katavi & Kapufi Ltd uliopo Mkoani Katavi mara baada ya kuwasili
mgodini hapo kwa ajili ya kujionea shughuli zinazoendelea mgodini hapo na
kuzungumza na wahusika masuala mbalimbali ya uendeshaji wa mgodi huo ikiwemo
hatua iliyofikiwa ya mgodi huo.
|
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa pili
kulia) akitembelea Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi Ltd uliopo Mkoani
Katavi ili kujionea shughuli ziazoendelea mgodini hapo.
|
Moja ya eneo la mitambo kwenye mgodi wa Dhahabu wa
Katavi & Kapufi Ltd uliopo Mkoani
Katavi.
|
No comments:
Post a Comment