Na Teresia Mhagama,
Kikao
hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam ambapo
wamezungumza masula mbalimbali kuhusu uendelezaji wa Sekta ya Madini nchini.
Waziri
Kairuki amesema kuwa mazungumzo yake na Balozi wa Kuwait yamelenga katika suala
la uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ambapo ameikaribisha nchi hiyo kuja
kuwekeza nchini ili kuendeleza Sekta husika.
Aidha,
ameongeza kuwa, katika kikao hicho wamezungumzia suala la kuwajengea uwezo
Wataalam wa Madini nchini ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Vilevile
wamejadiliana suala la kubadilisha uzoefu kati ya Kuwait na Tanzania lengo
likiwa ni kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inachangia ipasavyo katika uchumi wa
nchi husika.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akipokea
zawadi ya Ngao kutoka kwa Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem
(kulia), katika ofisi za Wizara ya
Madini jijini Dar es Salaam.
|
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akiwa
na Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kushoto), katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar
es Salaam.
|
No comments:
Post a Comment