Na Mohamed Saif,
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki amekutana na Mawaziri Wanne kutoka nchini Uganda
ambao wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya
kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa Sekta ya Madini.
Mawaziri
hao ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter, Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani,
Obiga Kania, Waziri wa Nchi- Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala, Namugwanya Bugembe na Waziri wa Nchi- Masuala
ya Uchumi, Dkt. Kasirivu Atwooki.
Waziri
Kairuki amekutana na ujumbe huo Novemba 28, 2017 katika Ofisi za Wizara ya
Madini jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali ya uendeshaji wa
shughuli za Madini nchini ikiwemo suala la Sera, Sheria na Kanuni za Madini
pamoja na masuala yanayohusu Wachimbaji Wadogo wa madini.
Ujumbe
huo utatembelea migodi mbalimbali ya Dhahabu inayomilikiwa na wazawa iliyoko
mkoani Geita ili kujionea uendeshaji wa migodi hiyo na hivyo kupata uzoefu wa
namna ya uendeshaji wake.
Aidha,
ujumbe huo wa Mawaziri kutoka nchini Uganda, utatembelea nchi mbalimbali Barani
Afrika ili kupata uzoefu wa usimamizi wa Sekta ya Madini hususan suala la
Wachimbaji Wadogo.
No comments:
Post a Comment