Na
Greyson Mwase, Simiyu
Oktoba
29, 2017
Wachimbaji
wa madini ya dhahabu katika wilaya ya
Maswa mkoani Simiyu wameiomba Serikali
kupitia Wizara ya Madini kufanya utafiti wa madini katika maeneo yao ili waweze
kuwa na uhakika wa uchimbaji wa madini
na uzalishaji wao kuwa na tija
Wameyasema
hayo leo tarehe 29 Oktoba, 2017 katika
ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo katika wilaya ya Maswa mkoani
Simiyu yenye lengo la kukusanya kero za wananchi mbalimbali hususan katika
shughuli za uchimbaji madini.
Akizungumza
kwa niaba yao, Sylivester Fundikira alisema kuwa wameunda jumla ya vikundi 30
ambapo kila kikundi kina mashimo yake na kueleza kuwa wamekuwa wakipata
changamoto ya upatikanaji wa madini ya
uhakika kutokana na maeneo yao kutofanyiwa utafiti kwa muda mrefu.
Akijibu
kero hiyo Naibu Waziri wa Madini
Stanslaus Nyongo alisema kuwa Wizara ya Madini kupitia Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST) imekuwa ikifanya tafiti
sehemu mbalimbali nchini na kusisitiza
kuwa Serikali kupitia Wizara ya
Madini ipo tayari kuwasaidia.
Alisema
Serikali inatambua mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo wa madini na kuongeza
kuwa imeweka mikakati ya kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini kwa
kuwapatia vifaa kupitia ruzuku ili
uchimbaji wao uwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
“
Tuna mpango wa kuhakikisha kuwa rasilimali za madini zinakuwa na mchango mkubwa
sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo
tutahakikisha tunasimamia ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa mazingira ya
uchimbaji madini yanakuwa rafiki,” alieleza Naibu Waziri Nyongo.
Katika
hatua nyingine, Nyongo alisema kuwa kazi yake pamoja na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ni
kuhakikisha kuwa sekta ya madini inakua kwa kasi na kuwa na mchango mkubwa
katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Alisema
kuwa sekta ya madini imekuwa na changamoto kubwa hususan katika upotevu wa
mapato kutokana na wawekezaji wasio
waaminifu na kukwamisha juhudi za serikali katika ukusanyaji wa mapato.
Aliendelea
kusema kuwa tangu Rais John Magufuli ameanza kupambana na wezi wa rasilimali za
madini kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwa uzalishaji na mapato umebadilika
kutokana na Serikali kuhakikisha kiwango sahihi kinapatikana na kulipiwa kodi
serikalini.
Alisema
Serikali imeweka Sheria Mpya ya Madini ya mwaka 2017 na kuwataka wachimbaji
madini nchini kufuata sheria hiyo pamoja na kanuni zake.
Mkuu
wa Wilaya ya Maswa, Seif Shekalaghe
akifafanua jambo mbele ya wakazi wa kitongoji cha Mwanguhi kilichopo wilayani
Maswa mkoani Simiyu (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
|
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, akijibu
kero mbalimbali za wakazi wa kitongoji cha Mwanguhi kilichopo wilayani Maswa
mkoani Simiyu (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
|
No comments:
Post a Comment