Mkazi
wa Kata ya Mbalagane iliyopo katika
wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Pulwa Sungwa akiwasilisha kero yake kwa Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara.
|
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo leo
tarehe 29 Oktoba, 2017 amefanya ziara ya
kikazi katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu lengo likiwa ni kukutana
na wananchi na kukusanya kero mbalimbali
hususan katika masuala ya madini. Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Seif
Shekalaghe pamoja na wataalam kutoka halmashauri. Ziara hii ni mwendelezo wa
ziara aliyoifanya katika mikoa ya Kagera
na Geita kwa ajili ya kufahamu shughuli za migodi ya serikali, binafsi na
wachimbaji wadogo.
No comments:
Post a Comment