Uchimbaji
wa madini ya dhahabu ukiendelea katika moja ya mashimo yanayomilikiwa na Mgodi wa Uchimbaji
Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo mkoani
Kagera.
Kaimu
Meneja Uchimbaji kutoka Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo, Rashil Rulanga
(kulia mbele) akielezea shughuli za uchimbaji zinavyofanyika katika mgodi huo
kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto mbele) mara alipofanya ziara
katika mgodi huo tarehe 27 Oktoba, 2017. Wa pili kushoto mbele ni Naibu Waziri
wa Madini, Stanslaus Nyongo.
Shughuli za utafiti wa madini ya dhahabu zikiendelea katika Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo uliopo mkoani Kagera.
Kutoka
kushoto mbele ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la
Taifa (STAMICO), Balozi Alexander Muganda,
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus
Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde wakiendelea na ziara
katika eneo la Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu
wa STAMIGOLD – Biharamulo.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati)
akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja Uchenjuaji kutoka Mgodi wa Uchimbaji
Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo,
Joseph Kamishina (kulia mbele) katika ziara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akifafanua jambo katika ziara hiyo.
Kaimu
Meneja Uchenjuaji kutoka Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo, Joseph
Kamishina(katikati) akielezea shughuli za uchenjuaji madini zinavyofanyika kwa
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) katika ziara hiyo. Kulia ni Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
Mmoja
wa wafanyakazi katika Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo, Sara Mkama
akiwasilisha kero yake kwa Waziri wa
Madini, Angellah Kairuki na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ( hawapo
pichani) mara Mawaziri hao walipokutana na watumishi wa mgodi huo kwenye ziara
hiyo lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua kero zao.
Sehemu
ya watumishi wa Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu
wa STAMIGOLD – Biharamulo, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Madini,
Angellah Kairuki (hayupo pichani)
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus
Nyongo (kulia) wakisikiliza kero mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na
watumishi mbalimbali wa Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo (hawapo pichani)
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwasilisha taarifa zote za
gharama za uendeshaji wa Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD –
Biharamulo ili kujiridhisha pamoja na kuchukua hatua za kisheria
iwapo kama kuna taratibu za manunuzi zimekiukwa.
Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 27 Oktoba, 2017 alipofanya ziara
katika mgodi huo uliopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera lengo likiwa
ni kufahamu shughuli za migodi ya serikali, binafsi na wachimbaji
wadogo.
Alisema kuwa gharama za uendeshaji wa shughuli za mgodi huo
zimekuwa ni kubwa mno pamoja na madeni hali inayopelekea shirika hilo
kujiendesha kwa hasara badala ya kujiendesha kwa faida.
Aliendelea kusema kuwa STAMIGOLD imekuwa ikitumia gharama kubwa
sana katika uendeshaji wa shughuli zake kwa kutumia mashine za kukodi na
kutaka watendaji wa mgodi huo kuwa wabunifu kwa kuibua mikakati mipya
kupunguza matumizi na kuzalisha faida kubwa ili hatimaye waweze
kutumia vifaa vyake badala ya kukodi.
“ Ukiangalia gharama inayotumika kukodi mashine za uchorongaji na
uchimbaji madini na nyinginezo utabaini kubwa sana ambapo kama STAMIGOLD
ingejipanga ingekuwa na uwezo kabisa wa kununa mashine na mitambo yake
yenyewe na kuepuka gharama kubwa za kukodi.
Aidha, Waziri Kairuki alielekeza Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na menejimenti ya Mgodi wa
STAMIGOLD kuwasilisha mpango wa kibiashara wenye kuainisha gharama za
uzalishaji, mapato na faida.
“ Tunataka kuanzia sasa STAMIGOLD uwe ni mgodi wa mfano wenye
kuzalisha kwa faida Tanzania, badala ya kufanya kazi kwa mazoea,”
alisema Kairuki.
Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki aliutaka Mgodi wa STAMIGOLD
kutumia Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kwenye tafiti zake za madini
kwa kuwa wakala huo una wataalam na maabara za kutosha.
Alieleza kuwa kutokana na wakala huo kuwa na uzoefu katika utafiti wa
madini ni muhimu kwa Mgodi wa STAMIGOLD kushirikiana nao kwenye utafiti
wa madini kama njia mojawapo ya kuboresha tafiti zake.
Naye Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliitaka STAMIGOLD
kuwa wabunifu kwa kufanya utafiti na kubaini maeneo yenye mashapo ya
madini ya dhahabu ili kuwa na miradi endelevu ya uchimbaji madini
Alisema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa sekta ya
madini inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi, hivyo inaanza
na usimamizi wa karibu kwa migodi yote inayosimamiwa na serikali,
binafsi na wachimbaji wadogo na kufanyia kazi changamoto mbalimbali
zinazojitokeza.
alipongeza ujio wa Waziri na Naibu Waziri wa Madini katika mgodi huo
na kuahidi kutekeleza kwa wakati maelekezo yaliyokuwa yametolewa.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Balozi Alexander Muganda
Alisema pamoja na mgodi kuwa na changamoto nyingi za kiuendeshaji
kama bodi watahakikisha wanasimamia masuala ya kiutendaji kwa karibu
zaidi, kushauri na kuwasilisha ripoti za mara kwa mara kwa Waziri na
Naibu Waziri wa Madini.
Wakati huo huo Waziri Kairuki pamoja na
Naibu wake Nyongo, walikutana na wafanyakazi wa Mgodi wa STAMIGOLD
Biharamulo ili kusikiliza kero mbalimbali na kuzitatua.
Katika kikao hicho Waziri Kairuki ameelekeza Bodi ya Wakurugenzi wa
Shirika la STAMICO pamoja na uongozi wa Mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo
kuzingatia maslahi ya watumishi ikiwa ni pamoja na kupata mishahara kwa
wakati, kuwa na bima za afya, kufuata utaratibu wa manunuzi na kuwepo
kwa uwazi kwenye uzalishaji.
Katika kikao hicho ameagiza bodi hiyo, kumsimamisha kazi aliyekuwa
afisa manunuzi, January Kinunda kwa kushindwa kusimamia mkataba wa
ukodishaji wa mashine kwa ajili uchorongaji.
Awali ilielezwa katika kikao hicho kuwa mashine hizo mbili zililetwa
kwa dharura huku zikiwa si mpya ambapo zimekuwa zikiharibika mara kwa
mara na kufikia hatua ya moja kufanya kazi mara moja kwa wiki na
kukwamisha uzalishaji katika
No comments:
Post a Comment