Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele
katikati) wakiongoza kikao na baadhi ya
wawakilishi kutoka Shirikisho la
Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa
Madini (FEMATA) mkoani Geita
Rais
wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA)
Taifa, John Bina (kulia) akieleza jambo
katika kikao hicho. Kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akifafanua jambo katika kikao hicho
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus
Nyongo wamekutana na wawakilishi kutoka Shirikisho la Vyama vya
Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA) mkoani Geita lengo likiwa ni
kubaini changamoto zao pamoja na kuzitatua. Kati ya maombi
yaliyowasilishwa na wawakilishi hao ni pamoja na uwepo wa siku ya
maadhimisho ya madini nchini, elimu kuhusu kanuni na sheria mpya za
madini, maeneo zaidi kwa ajili ya uchimbaji madini na fidia kwa wananchi
waishio ndani ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)
No comments:
Post a Comment