Na Issa Mtuwa,
Waziri wa Madini Doto Biteko
amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals
Ltd, ya Marekani, Rocky Smith na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni hiyo
Lucas Stanfield ofisini kwake Jijini Dodoma.
Watendaji hao wapo nchini kwa ziara
ya kawaida ya kikazi ya siku tano ambapo waliomba kukutana na Waziri wa
Madini.
Pamoja na mambo mengine, kampuni hiyo
inakusudia kuwasilisha taarifa juu ya hali na Maendeleo ya soko la dunia kwa
Madini ya Rare Earth Elements na kuzungumzia hatua iliyofikiwa kwa ombi la
leseni ya uchimbaji Mkubwa wa madini hayo.
Akizungumza katika kikao hicho,
Waziri Biteko amesema wizara iko tayari kuipokea kampuni husika nchini
baada ya kukamilika kwa taratibu kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu Rocky
Smith, amesema kuwa, amefurahishwa na ushirikiano unaooneshwa na wizara
na kuahidi kuanza shughuli za uchimbaji mara baada ya kukamilika kwa taratibu.
![]() |
Waziri wa Madini Doto
Biteko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals Ltd kutoka
Marekani Rocky Smith kushoto kwa Waziri. Smith alimtembelea Waziri ofisini
kwake jijini Dodoma kwa mazungumzo, wa kwanza kushoto ni Ali Ali, Kamishna
Msaidizi Uendelezaji Migodi na Madini Wizara ya Madini, anaefuatia ni
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Madini Edwin Igenge.
|
No comments:
Post a Comment