Na Greyson Mwase,
Waziri wa Madini,
Doto Biteko leo tarehe 06 Februari, 2019 amekutana na watendaji na watumishi wa
Tume ya Madini katika makao makuu ya Tume yaliyopo jijini Dodoma, lengo likiwa
ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Tume.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Madini, Profesa Simon Msanjila, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka
Wizara ya Madini, Issa Nchasi na
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.
Wengine ni pamoja na
Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, Katibu Mtendaji wa Tume
ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Wakurugenzi, Mameneja pamoja na watumishi
wa Tume ya Madini.
Katika kikao hicho
Waziri Biteko ametoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vituo vya ukaguzi
wa madini ya ujenzi kufufuliwa, kikao cha kamati tendaji kukutana mara kwa mara
kwa ajili ya kupitia na kuidhinisha maombi mbalimbali ya leseni za madini na
watumishi kufanya kazi kwa uadilifu.
Waziri wa Madini,
Doto Biteko (katikati) akisikiliza mapendekezo mbalimbali yaliyokuwa
yanawasilishwa na watumishi wa Tume ya Madini (hawapo pichani)
Waziri wa Madini,
Doto Biteko akizugumza na watumishi wa Tume ya Madini (hawapo pichani).
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Madini, Profesa Simon Msanjila akifafanua jambo katika kikao hicho.
Katibu Mtendaji wa
Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akiwatambulisha viongozi wa Tume ya
Madini pamoja na wafanyakazi.
Watumishi wa Tume ya
Madini wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko
(hayupo pichani)
Watumishi wa Tume ya
Madini wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko
(hayupo pichani)
Watumishi wa Tume ya
Madini wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko
(hayupo pichani)
No comments:
Post a Comment