Na Asteria Muhozya,
Kufuatia kukaidi Wito
wa kuonana na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa
Richard Kasesela kutokana na kufanya ununuzi haramu wa madini
ya dhahabu ikiwemo kufadhili uchimbaji haramu, Naibu Waziri Nyongo amevitaka
vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Iringa
kuwakamata Mansoor Almasi na Jacob
Mwapinga iwapo watashindwa kuripoti wenyewe katika Mamlaka zinazohusika.
Naibu Waziri Nyongo
ametoa agizo la kukamatwa wahusika hao baada ya kukiuka agizo la kuonana na
viongozi hao kwa hiari ambapo
walielekezwa kuonana na Naibu Waziri na Mkuu wa Mkoa Januari 15.
Pia, kabla ya wito wa
Naibu Waziri, awali, wahusika hao walitakiwa kuonana na Mkuu wa Wilaya ya
Iringa wakiwemo Maafisa Madini kwa ajili ya kuupatia suluhisho mgogoro huo katika
mgodi wa dhahabu wa Ulata, kijiji cha Ulata wilaya ya Iringa unaomilikiwa na
Ibrahimu Msigwa.
Naibu Waziri Nyongo
alibaini kuwa Mansoor na Mwapinga wanafanya ununuzi wa madini kinyume cha Sheria ikiwemo kufadhili shughuli za uchimbaji katika mgodi ambao siyo
wamiliki wake.
Pia, Naibu Waziri
ameelekeza baada ya wahusika hao
kukamatwa wanatakiwa kutoa maelezo kueleza ni lini watalipa kodi wanazodaiwa na
serikali baada ya kufanya shughuli hizo
bila kulipa kodi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wachimbaji hao,
Naibu Waziri Nyongo aliwaeleza kuwa, Serikali inamtambua Ibrahimu Msigwa kama
mmiliki halali baada ya kuwa na vibali vya kumiliki leseni ya mgodi huo na
hivyo kutoa wito wa kuonana na pande zote ili kuhakikisha kuwa anatoa suluhisho la mgogoro uliopo baina
ya Msigwa, Mansoor, Mwapinga na wachimbaji.
Akihitimisha ziara
yake mkoani Iringa Januari 15, Naibu Waziri Nyongo amesema kuwa, amebaini
ukwepaji mkubwa wa kodi katika migodi ya
Ulata na Nyakavangala.
Amesema wamiliki wa
leseni wanaotumia mrabaha kwa ajili ya kufanya masuala mengine ya kijamii
wanakiuka taratibu na kueleza kuwa, fedha za kufanyia shughuli za maendeleo
zinapaswa kutoka katika fedha za Uwajibikaji kwa jamii ambazo halmashauri
zinapanga kupitia Baraza la Madiwani.
Kwa upande wake, Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema wahisika Mwapinga na Almasi wana kiburi na kwamba
waliitwa kwa ajili ya kuongea ili ku[ata fursa ya kujieleza na a kueleza ni lini
watalipa mrabaha lakini wamekaidi hivyo
kinachofuatia ni wahusika kukamatwa.
Naibu Waziri Nyongo
alifanya ziaea katka mgodi wa Ulata Janauri 14 akilenga kukagua shughuli za
uchimbaji madini katika mgodi huo ikiwemo kutatua mgogoro uliokuwep katika mgodi
huo baina ya mmiliki halali Ibrahimu Msingwa, wanunuzi haramu
wa madini hayo Mansoor Almasi na Jacob Mwapinga.
Naibu Waziri wa
Madini Stanslaus Nyongo, akikagua moja ya mgodi
katika mgodi wa Nyakavangala wakati wa ziara yake mgodini hapo. Wa tatu
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
|
Naibu Waziri wa
Madini Stansaus Nyongo akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua mgodi
wa Nyakavangala. Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
|
Mkuu wa Wilaya ya
Iringa Richard Kasesela akimwonesha jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo wakati wa ziara yake ya kukagua migodi ya Nyakavangala.
|
No comments:
Post a Comment