Wednesday, October 17, 2018

Waziri Kairuki akabidhiwa kikombe cha ushindi, maonesho ya viwanda, Geita


Wizara ya Madini ilikuwa Mshindi wa Kwanza katika Taasisi za Serikali zilizoshiriki Maonesho ya Kwanza ya Teknolojia ya Uchimbaji na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu yaliyofanyika Mkoani Geita kuanzia mkoani Geita tarehe 24 – 30 Septemba, 2018.

Maonesho hayo yalifunguliwa kwa niaba ya Waziri wa Madini na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na kufungwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.


Waziri wa Madini Angellah Kairuki,  (kushoto) akikabidhiwa Kikombe cha Ushindi na Cheti cha Ushiriki wa wizara katika Maonesho ya Kwanza ya Teknolojia ya Uchimbaji na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kulia). Katikati ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa.

No comments:

Post a Comment