·
Ataka migodi
mingine nchini kuiga mgodi huo
Na Greyson Mwase, Songea
Naibu
Waziri wa Madini, Dotto Biteko amepongeza utendaji kazi wa mgodi wa kuzalisha
makaa ya mawe wa Kambas uliopo wilayani Songea mkoani Ruvuma na kuitaka migodi
mingine nchini kuiga mfano kwenye uchimbaji madini kutoka kampuni hiyo.
Biteko
ameyasema hayo leo tarehe 17 Julai, 2018
kwenye ziara yake aliyoifanya katika mgodi huo uliopo katika kijiji cha Maniamba wilayani Songea mkoani Ruvuma, lengo
likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji madini katika mgodi huo pamoja na
kutatua changamoto zilizopo.
Katika
msafara wake aliambatana na wataalam kutoka Wizara ya
ya
Madini, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, Maafisa Madini wa Songea,
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama
vya Wilaya ya Songea.
Mara
baada ya kupokea taarifa ya shughuli za uchimbaji madini katika mgodi huo
kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mgodi huo, Yahya Yusuph Kambaulaya, Naibu Waziri
Biteko aliuopongeza mgodi huo kwa kuweza kuzalisha makaa ya mawe na kuuza ndani
ya kipindi kifupi tangu imeanza uchimbaji wake Desemba mwaka 2017.
Aidha,
aliutaka mgodi huo kuunganisha leseni zake 14 za madini ili kuweza kuwa wachimbaji wa kati hatimaye
kuwa wachimbaji wakubwa na kuzidi kuongeza mapato Serikalini.
“Kampuni hii imeanza baada ya Sheria Mpya ya Madini ya mwaka 2017 ambayo ni
rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, ndani ya kipindi kifupi wameanza
kuchimba kwa mafanikio makubwa, kutoa ajira kwa wazawa na kushiriki katika
shughuli za huduma za jamii ( corporate social responsibility), nazitaka
kampuni za madini zote nchini kuiga
mfano wa kampuni hii,” alisema Biteko.
Aliendelea
kusema kuwa, ni matarajio yake kuona
mgodi wa Kambas unazidi kukua na kuitaka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Halmashauri ya Songea, na Afisa Madini kuulea
mgodi huo huku wakihakikisha unafuata sheria na kanuni za madini.
Aidha
Biteko alitaka halmashauri kutumia fedha inazopata kama mapato kwenye mgodi huo
kwenye uwekezaji mwingine mbadala kama vile shule, vituo vya afya na barabara
ili kuacha kumbukumbu nzuri katika vizazi vijavyo.
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko aliutaka mgodi wa Kambas kulipa kodi
stahiki serikalini mara baada ya kufanyika kwa mauzo kwenye kituo cha mwisho (gross
value) badala ya mauzo ya hapo hapo mgodini (net back value).
“Sheria
ya Madini ya Mwaka 2010 kifungu cha 87 (6) kinaeleza kuwa kodi ya madini
itakokotolewa baada ya bei ya mwisho nje ya nchi kule yanapouzwa madini hayo na
si hapa mgodini, hivyo ninaona ni vyema niwaambie mapema ili kusijitokeze
kasoro baadaye,” alisisitiza Biteko.
Aidha,
Biteko aliwataka wananchi walioajiriwa katika mgodi wa Kambas kufanya kazi kwa
uadilifu mkubwa na kutoa ushirikiano kwa mwekezaji huyo mwenye nia ya dhati ya
kuwasaidia wananchi hao.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mdeme mbali na kumpongeza Naibu Waziri Biteko
kwa usimamizi makini wa sekta ya madini
nchini aliongeza kuwa, ofisi yake ipo tayari kushirikiana na mwekezaji huyo
pamoja na kutatua changamoto zitakazojitokeza.
Awali,
akiwasilisha taarifa ya uzalishaji, Mtendaji Mkuu wa Mgodi wa Kuzalisha Makaa
ya Mawe wa Kambas, Yahya Yusuph Kambaulaya alisema kuwa uzalishaji wa makaa ya
mawe katika mgodi huo umekuwa ukiongezeka siku hadi siku ambapo mpaka sasa
wameshachimba tani 5138.
Alifafanua
kuwa tani hizo zilichimbwa kwa muda wa miezi mitatu ya Desemba 2017, Mei, 2018
na Juni, 2018 na kuendelea kufafanua kuwa kati ya kipindi cha Januari hadi
Aprili, 2018 shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe zilisimama kutokana na mvua
kubwa.
Aliendelea
kusema kuwa, kuanzia Julai 2018 uzalishaji wa makaa ya mawe kwa siku ni tani
200 na kusisitiza kuwa malengo ya mgodi ni kuzalisha tani 600 hadi 700 kwa siku ambapo kwa mwezi
mgodi utakuwa na uwezo wa kuzalisha kati ya tani 18,000 hadi 21,000.
Akielezea
manufaa ya mgodi wa Kambas, Kambaulaya alisema mgodi umeweza kulipa serikalini
kodi mbalimbali inayotokana na mauzo ya makaa ikiwa ni pamoja na mrabaha na ada
ya ukaguzi shilingi milioni 16, shilingi milioni 4.1 katika kijiji cha Maniamba
kama mchango kwa huduma za jamii.
Alisema
pia mgodi wake ulichangia katika huduma za kijamii katika ujenzi wa Shule ya
Msingi Mipeta iliyoezuliwa paa na upepo mwezi Desemba, 2017 kwa kutoa vifaa vya
viwandani vyenye thamani ya shilingi milioni tano na ukarabati wa ofisi ya
kijiji cha Maniamba kupitia vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni
nne.
Kambaulaya
aliendelea kusema kuwa mgodi wa Kambas pia umefanikiwa kutoa ajira 20 rasmi na
zisizo rasmi 50 hivyo kukuza uchumi wa wananchi wanaozunguka mgodi.
Akielezea
maratajio ya mgodi wa Kambas, Kambaulaya alisema mgodi unatarajia kupanuka
zaidi kwa kuanzisha mchakato wa uzalishaji wa umeme unaotokana na makaa ya mawe
kwa kushirikiana na kampuni ya BBIC kutoka Chini ambapo mpaka sasa wameshasaini
makubaliano ya awali ya namna ya kujenga mtambo
wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe wenye uwezo wa Megawati 500
hadi 1000 ambapo umeme huo utaingizwa
kwenye Gridi ya Taifa.
Aidha,
akielezea changamoto za mgodi huo Kambaulaya alieleza kuwa ni pamoja na
miundombinu ya barabara kutokuwa rafiki katika usafirishaji wa makaa ya mawe na
kutafuta njia sahihi ya kuongeza uzalishaji wa makaa ya mawe kulingana na
tabaka la makaa yanayopatikana katika eneo hilo.
Mhandisi
Uchimbaji wa Mgodi wa Kambas, Himid Didi (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu
Waziri wa Madini, Dotto Biteko (katikati).
|
Naibu
Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza na watumishi pamoja na watendaji wa
Mgodi wa Kambas.
|
Shughuli
za uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe zikiendelea katika Mgodi wa Kambas.
|
No comments:
Post a Comment