Na
Veronica Simba, Dodoma
Wafanyakazi wa Wizara
ya Nishati na Wizara ya Madini, walioko Makao Makuu Dodoma, wameungana na
wenzao duniani kote kuadhimisha sikukuu ya Mei Mosi.
Katika kuadhimisha
sikukuu hiyo muhimu, wafanyakazi hao walishiriki maandamano yaliyoanzia katika
viwanja vya bunge na kuhitimishwa katika uwanja wa Jamhuri, ambapo walipokewa
na Mgeni Rasmi; Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge.
Pamoja na mambo
mengine yaliyofanyika wakati wa sherehe hizo, wafanyakazi bora walipatiwa
zawadi na vyeti vya kutambua mchango wao.
Baadhi ya Wafanyakazi
bora kutoka Idara mbalimbali za Wizara ya Nishati ni Mwamvita Mkakile kutoka
Idara ya Nishati, Margaret Vava (Utawala) na Vera Sikana (Sera na Mipango).
Taratibu za kuwapata wafanyakazi bora wengine kutoka Idara zilizosalia
zinakamilishwa ili waweze kupatiwa vyeti pamoja na zawadi zao.
Kwa upande wa Wizara
ya Madini, wafanyakazi bora ni Happy Ndunguru kutoka Idara ya Utawala ambaye
pia ndiye mfanyakazi bora wa Wizara. Wengine ni Eugenia Mashoko (Uhasibu),
Godfrey Nyamsenda (Sheria), Zuwena Msuya (Mawasiliano Serikalini), Josephat
Mbwambo (Sera na Mipango), Christopher Mwita (TEHAMA), Dorothy Mtweve (Madini),
Eric Kwesigabo (Ugavi) na Hassan Ngwandu (Ukaguzi wa Ndani).
Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini waliopo Makao Makuu Dodoma, wakishiriki maandamano ya Mei Mosi, 2018. |
Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini waliopo Makao Makuu Dodoma, wakishiriki maandamano ya Mei Mosi, 2018. |
Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini walioko Makao Makuu Dodoma, wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa maadhimisho ya sherehe ya wafanyakazi (Mei Mosi). |
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini walioko Makao Makuu Dodoma, wakiwa katika Ofisi za Wizara, muda mfupi kabla ya kuanza maandamano ya sherehe ya wafanyakazi (Mei Mosi). |
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini walioko Makao Makuu Dodoma, wakiwa katika Ofisi za Wizara, muda mfupi kabla ya kuanza maandamano ya sherehe ya wafanyakazi (Mei Mosi). |
No comments:
Post a Comment