Na Asteria
Muhozya,
Waziri wa
Madini Doto Biteko amewasili Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma na kupokelewa
na Watumishi wa Wizara ya Madini na baadhi ya Taasisi zake.
Akizungumza na
watumishi hao, amewataka kujipanga na kushirikiana pamoja na viongozi wa wizara
na kuongeza kuwa, wao kama viongozi wanawategemea sana watumishi kuweza
kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
“Mimi sio
mgeni ni mwenyeji, wote tunafahamiana.
Nawashuru kwa kutupokea mimi na mwenzangu Nyongo. Ninyi ndiyo wenye wizara
sisi hatuwezi kuwa hapa kama ninyi hamjatupa ushirikiano,” amesema Biteko.
Waziri wa Madini, Doto Biteko
akizungumza na watumishi wa wizara ya Madini mara baada ya kupokelewa wizarani hapo, kufuatia kushika wadhifa Mpya
wa kuwa Waziri wa wizara hiyo.
Watumishi
wa Wizara ya Madini wakimkaribisha Waziri wa Madini Doto Biteko katika wizara
hiyo mara baada ya kuwasili kutoka kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Sambamba ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
Waziri
wa Madini, Doto Biteko akipokea maua kutoka kwa Afisa kutoka Wizara ya Madini
Dorice Kagya mara baada ya kuwasilili katika ofisi za wizara Sambamba naye ni
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
Watumishi
wa Wizara ya Madini wakimkaribisha Waziri wa Madini Doto Biteko katika wizara
hiyo mara baada ya kuwasili kutoka kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Sambamba ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
Waziri
wa Madini, Doto Biteko akipeana mkono na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
watu, Issa Nchasi kama ishara ya kumkaribisha tena kushika katika wadhifa mpya
baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
John Magufuli.
Waziri
wa Madini, Doto Biteko akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof.
Simon Msanjila alipowasili katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Kikuyu jijini
Dodoma. Sambamba naye ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu, Issa Nchasi na watumishi wengine wa wizara.
No comments:
Post a Comment