v Aeleza itafika kokote madini
yanakochimbwa pasipo vibali halali
Na
Nuru Mwasampeta
Naibu Waziri wa
Madini, Doto Biteko amewaeleza watanzania wasiofuata Sheria katika utafutaji,
uchimbaji na biashara ya madini nchini kuwa Serikali inaona na itafika popote
madini yanapochibwa pasipo vibali halali vya kufanya shughuli hiyo.
Biteko ameyasema hayo
mwishoni mwa wiki, Tarehe 5 mwezi Januari, 2019 alipofanya ziara ya kukagua
eneo ambako shughuli za uchimbaji wa madini ya shaba ulifanywa pasipo kibali na
kubaini viashiria vya uchimbaji katika hifadhi ya Wanyama pori ya Makao iliyopo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.
Akizungumzia lengo la
ziara hiyo, Biteko alisema kumekuwa na viashiria vya kuwepo kwa watu wasiokuwa waaminifu
na kujiingiza katika shughuli ya uchimbaji pasipokuwa na vibali jambo ambalo
halikubaliki na halitavumilika. “Sisi madini yanatuuma, tukisikia kuna watu
wanachimba tutafika mahali popote kujua madini hayo yanachimbwa na kupelekwa
wapi” Biteko alikazia.
Aliendelea kwa
kusema, huu mchezo ulifanyika sana na sasa nimekuja kuwaambia hautajirudia
tena. Endapo mtu yeyote anataka kuchimba madini ya yoyote ikiwa ni pamoja na madini
ya ujenzi kama vile mchanga wa kutengenezea barabara sharti afike katika ofisi
zetu za madini aeleze nia na eneo analotakiwa kutengeneza barabara na wahusika
watamuonesha eneo la kuchimba mchanga kwa utaratibu wa kisheria kwa matumizi
hayo si kujiamlia tu.
Biteko alisisitiza kuwa
lengo la ziara hiyo si kutoa kibali kwa watu kuchimba katika hifadhi hiyo. “Sisi hatujaja kupromote watu wachimbe bali tumekuja kwa sababu watu wanachimba
pasipo taratibu.
Alibainisha kuwa ili
mtu yeyote apate kibali cha kuchimba katika hifadhi hiyo sharti apate kibali
kutoka mamlaka kuu nne ambazo ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji
kwa sababu katika hifadhi hiyo kuna vyanzo vya maji, Mamlaka ya Mazingira
(NEMC)pamoja na Wizara ya Madini.
Katika ziara hiyo ya
kushtukiza Biteko aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon
Msanjila aliyeelezea sheria na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili mtu yeyote
kuweza kujihusisha na shughuli za Madini.
Aidha, Profesa
Msanjila aliwataka watanzania kujua kuwa rasilimali madini zinazopatikana
nchini ni kwa manufaa ya watanzania wote hivyo ni lazima wafuate utaratibu ili
mapato yatokanayo na tozo mbalimbali kutokana na utafiti, uchimbaji na biashara
ya madini ziwanufaishe watanzania wote. “Lazima niwaambie haya madini ni ya
watanzania wote” alikazia.
Akizungumzia chanzo
cha taarifa ya kuwepo kwa uchimbaji katika hifadhi hiyo Leons Welenseile
(Mjiolojia) alisema mnamo mwaka 2016 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alifanya ziara
iliyolenga kutatua mgogoro baina ya kampuni ya inayomiliki leseni ya uwindaji
wanyamapori katika hifadhi hiyo Mwiba Holdings Limited na wananchi wanaozunguka
hifadhi hiyo baada ya wananchi kutoridhishwa na kile walichokuwa wakikipata
kutoka kwa mwekezaji huyo.
Walipokuwa njiani
kutoka katika kusuluhisha mgogoro huo ndipo wataalamu wa madini katika mkoa huo
walikutana na loli lililobeba mchanga pasipokuwa na vibali halali vya kufanya
uchimbaji huo nakubaini kuwa shughuli
hiyo ilikuwa ikifanywa na kampuni hiyo ya mwiba kwa lengo la kukarabati
barabara katika hifadhi hiyo pasipo kujua kuwa walipaswa kuwa na leseni ya kuchimba
mchanga huo na kupigiwa hesabu iliyopelekea kulipa mrabaha wa milioni 50 baada
ya kukiri kufanya shughuli hiyo kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani alikiri kutokuwa na taarifa za
uchimbaji huo na kuwataka wataalamu na maafisa madini katika eneo lake kutoa
taarifa pindi masuala ya ukiukwaji wa taratibu na sheria za nchi yanapotokea
katika eneo lake ili kuweza kushirikiana katika kutatua changamoto hizo.
Wajumbe walioambatana
na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Simon
Msanjila, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani katika hifadhi
ya wanyama ya Makao wilayani Meatu mkoani Simiyu.
Pori kwa pori
mbugani, Prof. Simon Msanjila akiongoza wajumbe walioambatana kujiridhisha,
kukagua pamoja na kutoa kauli ya serikali kwa wafanya biashara wa madini
wanaojihusisha na biashara hiyo kinyume na taratibu na sheria ya nchi, Nyuma
yake mwenye suti ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani
Naibu Waziri wa
Madini Doto Biteko (wa pili) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon
Msanjila wakitoka katika jengo la ofisi za mwekezaji wa hifadhi za wanyamapori
ya Makao, Mwiba Limited kuelekea eneo linalosadikiwa kuendesha shughuli za
Uchimbaji hifadhini humo.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani akiongea jambo mara baada ya kupokea ugeni
kutoka Wizara ya Madini katika wilaya yake ya Meatu
|
Baadhi ya wanyama
wanaoonekana katika hifadhi ya wanyama ya Makao katika Wilaya ya Meatu Mkoani
Singida
|
No comments:
Post a Comment