Na
Nuru Mwasampeta
Naibu Waziri wa
Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuzingatia uchimbaji
salama ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara katika maeneo ya migodi.
Ametanabaisha kuwa akifa mtanzania mmoja huyo Mtanzania ni muhimu kuliko mgodi
wote, ‘kuliko mtanzania mmoja afe ni bora huo mgodi usiwepo’.
Aliyasema hayo leo
tarehe 04 mwezi Januari alipokuwa akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo katika
eneo la uchimbaji mji wa Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara inayoendelea kwa
siku mbili.
Biteko alibainisha
kuwa, Buhemba ni eneo linaloongoza kwa ajali kwenye migodi, huu mgodi ulifungwa
na toka umefunguliwa kuna vifo vya wachimbaji kumi na mbili na majeruhi 20,
Serikali haiwezi ikakubali hali hiyo iendelee “Mimi nakwambia mwenyekiti
sitakubali hali hii iendelee mimi mwenyewe nitakuja kuufunga tena mgodi huu
kama hali hiyo itaendelea hatuwezi kupoteza maisha ya watanzania” Biteko
alisisitiza.
Biteko aliongeza kwa
kusema, Serikali haiko tayari kuona kuwa watu wanaendelea kufa ndio maana
imeamua kufika na kuandaa mafunzo kwa
ajili ya wachimbaji wadogo ili waweze
kufundishwa namna bora za uchimbaji salama na wenye tija.
Biteko alisema
mafunzo hayo yanalenga kuwafundisha wachimbaji wadogo masuala ya uchimbaji salama,
uchenjuaji, afya, na mazingira ya uchimbaji katika mkoa huu wa Mara.
Akiwapongeza wananchi
na wachimbaji wadogo wa madini Buhemba, Biteko alisema kumetokea ugonjwa mmoja
kwa watanzania wa kukwamisha mradi wa Serikali,
wananchi wanaanza vurugu na kudai fidia lengo ikiwa ni kukwamisha tu
utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa watanzania lakini Buhemba mmeonesha
ushirikiano mkubwa kutoka mwanzo mpaka mwisho wa utafiti.
Aidha, Biteko
alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa ushirikiano anaoufanya katika kusimamia shughuli
za uchimbaji wa madini. Amesema mara nyingi wachimbaji wadogo wanakuwa kama
watoto yatima lakini si kwa hapa Buhemba. Hawana mlezi, wanajiendesha wenyewe
na wakati mwingine mamlaka za serikali zinajitokeza pindi matatizo yanapotokea
lakini Mkuu wa wilaya amekuwa bega kwa bega.
Aidha, Biteko
aliwasihi wachimbaji wadogo wa Buhemba kuchangia kwa ukamilifu katika pato la
taifa. Alisema wakati wote ukikutana na kesi ya utoroshwaji wa madini mhusika
mkuu anakuwa ni mchimbaji mdogo. Aliendelea kwa kuwaeleza wachimbaji hao kuwa
wamepata Rais ambaye anawapenda, anawajali anawadhamini, Rais anayependa wachimbaji wadogo wahame kutoka kwenye daraja
la chini na kuwa watanzania wanaofurahia maisha kwenye nchi yao kwa kuthaminiwa na kuheshimiwa, “nilidhani
zawadi pekee ambayo mngeipa Serikali na Rais wetu DKt ni nyie kusimamiana
mkalipa kodi vizuri, mhame kwenye mfumo wa kukwepa kodi na kutorosha madini”.
Biteko alisisitiza
Pamoja na hayo Biteko
alibainisha kuwa, katika mkoa wa Mara wilaya inayoongoza kwa kulipa kodi ni
wilaya ya Butihama, alisema kiasi cha milioni 57 za kitanzania zimelipwa kwa
mwezi jana, hata hivyo aliwahimiza wachimbaji hao kufanya zaidi ili kuipa serikali wajibu mkubwa
wa kuwahudumia.
“Ninapima mapenzi ya
Rais Kwenu, halafu ninapima kile mnachochangia ninyi kwenye pato la Taifa
haviendani” Mimi nilidhani mtu anayekupenda nawewe unamlipa kwa kumpenda zaidi.
Rais wetu anawapenda wachimbaji wadogo hataki mtangetange, mpeni sababu ya
kuendelea kuwapenda, mpeni sababu ya kuendelea kuwahudumia, siku mtu akiwagusa
Rais awateteee kutokana na kodi zenu”
Naomba sana muwe
wazalendo, muwe waaminifu, ili mchango wenu katika sekta hii uweze kuonekana na
kutumika katika maeneo mengine nchini. Ili Serikali iweze kuhudumia maeneo
mengine kama vile elimu, afya, usafirishaji na mambo mengine ni kutoka katika
kodi. Simamianeni ninyi kwa ninyi, onyanenyi ninyi kwa nini bora mtu mbaya bora
ake nje ya sekta.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Mara (MAREMA) Dave Bita alitoa shukrani
zake za dhati kwa serikali kwa kutupa jicho kwa wachimbaji wadogo kwa lengo la kuwawezesha kuwa na uchimbaji wenye tija.
Aliishukuru Serikali kwa kujipanga kuwajengea kituo cha mafunzo kwa ajili ya
kuboresha na kuimarisha masuala ya utafutaji na uchimbaji wa madini.
Ameishkuru Serikali
kwa kuwasilisha taarifa ya utafiti ulioanza mwezi Oktoba 2016 kwa wachimbaji wa
Butiama matokeo yatakayowapelekea kunufaika na uchimbaji wao.
Aidha, Dave amewataka
wachimbaji wadogo kutengeneza mazingira ya kukubali kuwalipa posho viongozi wanaowasimamia
katika shughuli zao vinginevyo wataendelea kugombana na viongozi hao siku kwa
siku na hata kupelekea migogoro. Amesema wachimbaji wadogo hawako tayari
kuwalipa viongozi wanaowasimamia katika maeneo ya uchimbaji.
Aidha, amewasihi
wachimbaji wadogo kutumia mafunzo yanayotolewa kwa manufaa ameomba watoe
ushirikiano kwa voiongozi watakaowachagua pamoja na kuwasihi kukitumia kwa
manufaa kituo cha mafunzo kinachojengwa na serikali kwa ajili yao.
Naibu Waziri wa
Madini, Doto Biteko akizungumza jambo akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Butiama Annarose Nyamubi (Hayupo pichani) juu ya uwepo wake wenye lengo la
kufungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini wa Mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa
Madini, Doto Biteko (aliyekaa kushota) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria mafunzo ya namna bora ya kujikita
katika uchimbaji wenye tija.
Baadhi ya Wachimbaji
wadogo waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao yenye lengo la
kuboresha sekta ya uchimbaji mdogo wa Madini yanayoendelea katika wilaya ya
Butiama mjini Buhemba mkoani Mara.
Mkuu wa Wilaya ya
Butiama, Annarose Nyamubi (aliyesimama) akieleza jambo mbele ya Naibu Waziri wa
Madini, Doto Biteko (Kushoto) alipofika ofisini kwake kuelezea uwepo wake
katika wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment