Na
Nuru Mwasampeta,
Katika kutekeleza
ilani ya Chama cha Mapinduzi na utekelezaji wa ahadi za chama kwa wananchi,
Naibu Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki
Stanslaus Nyongo leo amekagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo
lake.
Nyongo alitembelea
mradi wa ujenzi wa shule unaoendelea katika kata ya Nyalikungu na kuagiza shule
hiyo ya msingi ianze kupokea wanafunzi
kuanzia mwezi huu ili kuwapa nafuu wanafunzi wanaotembea mwendo mrefu kutafuta
elimu.
Aidha, Nyongo
ameelekeza mwenge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakapopita katika wilaya
ya Maswa, ndipo shule hiyo ifunguliwe rasmi ili kuruhusu masuala mengine ya
kimaendeleo kutekelezwa.
Mara baada ya
kukamilisha ukaguzi katika eneo hilo, Nyongo alielekea katika kijiji cha ambako alikagua maendeleo ya ujenzi wa
zahanati ambao haukuwa wakuridhisha aidha, alitembelea hospitali ya Wilaya ya
Maswa kujionea eneo lililopendekezwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Mama na
Mtoto ambalo mchakato wa ujenzi na upatikanaji wa pesa umekamilika.
Akizungumzia
changamoto wanazokutana nazo katika eneo hilo la shule, Diwani wa Kata ya
Nyalikungu, Joseph Bundara, alisema ni kutokuwa na barabara, huduma ya maji,
umeme pamoja na ombi lakujengewa nyumba ya mwalimu ili kuishi karibu na
mazingira ya shule.
Akizungumza wakati wa
ukaguzi wa mradi wa shule iliyopo katika kata hiyo ya Nyalikungu Katibu wa CCM
wilaya ya Maswa Mwl. Mathius Filagisa alimtaka Diwani wa kata hiyo kuhakikisha
wakati wa ziara za viongozi wa juu wa Chama na CCM viongozi wote na watendaji
wote wa Serikali wawepo katika ziara na mikutano ili kujibu hoja zitakazoibuka wakati wa
mikutano hiyo.
Tunatekeleza Ilani ya
CCM kuleta makaimu kwenye ziara za waheshimiwa haifai mjitahidi mwaunge mkono
viongozi wenu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao wawapo majimboni” alikazia.
Naibu Waziri wa
Madini Stanslaus Nyongo (kulia) akiambatana na wajumbe wa Chama na mhandisi wa
barabara akikagua ujenzi wa Barabara ya km 1.5 ikiwa ni moja ya ahadi za chama
|
No comments:
Post a Comment