Ø Ni baada ya kufungwa kwa miezi
Mitano
Ø Biteko azidua Ofisi ya Madini
Ulanga
Na Rhoda James, Mahenge
Naibu Waziri wa
Madini, Doto Biteko ameufungua mgodi wa Wachimbaji Wadogo wa Mahenge baada ya
kufungwa kwa takribani miezi Mitano tangu
Julai 10, 2018.
Mgodi huo wa madini
ya Vito aina ya Spino uliopo Wilayani
Ulanga ulisimamishwa kutokana na kukiukwa kwa taratibu za uchimbaji wa madini
ikiwemo kutolipa kodi za Serikali.
Akizungumza katika
mkutano kati yake na wachimbaji Biteko alisema kuwa, Sekta ya Madini haipo kwa
ajili ya kufunga migodi, na kuongeza kuwa, hakuna mchimbaji yeyote
atakayeruhusiwa kuchimba katika eneo hilo hadi pale atakapokuwa amelipa madeni
yake angalau ya awamu ya kwanza.
Pia, alisema kuwa,
ikiwa kuna mchimbaji ambaye atakiuka taratibu za uchimbaji, atachukuliwa hatua
za kisheria na si kwa kufungiwa mgodi tu
bali atapelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
“Nyie ni wadau muhimu katika sekta ya
maendeleo, na mkilipa kodi, ikaonekana imefanya nini, hata wawekezaji
hawatakwepa kulipa kodi,” alisema Biteko.
Aliwataka Wachimbaji
Wadogo wa Mahenge kubadilika na kufuata taratibu zilizowekwa kisheria na kusema
kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano haitaki rushwa hususan kwenye Sekta ya Madini.
Aidha, pamoja na kufuungua
mgodi huo, Biteko pia alizidua Ofisi ya Afisa
Madini Mkazi wa Mahenge, ikiwa ni mojawapo ya mahitaji ya awali ili
shughuli za uchimbaji madini katika Mji wa Mahenge ziende kama inavyotakiwa.
Pia, Biteko alimtaka
Afisa Mkazi wa Mahenge, Tandu Jirabi kuhakikisha leseni za dealers zinasainiwa ili
pamoja na kutoa utaratibu kwa wadau hao kuhusu namna ambavyo wanatakiwa
kutekeleza majukumu yao kabla ya
kupatiwa leseni.
“Mzawa lazima awe na
mashinetano na mwekezaji kuwa na mashine 30,” alisema Biteko.
Aidha, Biteko alitoa
wito kwa viongozi wa Halmashauri ya Mahenge kuhakikisha kuwa fedha zinazolipwa
kama kodi zinatumika ipasavyo katika kuwezesha huduma mbalimbali za jamii
ikiwemo kujenga Zahanati, Shule, Barabara na kadhalika.
Kwa Upande wake,
Mbunge wa Jimbo la Mahenge Goodluck Mlinga alimshukuru Naibu Waziri Biteko kwa
kufugua mgodi huo wa wachimbaji wadogo na kuwataka wananchi wa Mahenge kufuata
taratibu zinazotakiwa ili kuepusha usubufu kama huo uliojitokeza hapo awali.
Mlinga alisisitiza kuwa, kodi inayolipwa na
Wachimbaji Wadogo lazima itekeleze majukumu yaliyopangwa na kumwakikishia Naibu
Waziri kuwa wachimbaji watalipa kodi kwa kishindo.
Naye, Mkuu wa Wilaya
ya Ulanga, Ngollo Malenya alisema kuwa Rais Magufuli anataka kila mwananchi
afaidike na rasilimali za madini, hivyo, kuwataka wananchi na Wachimbaji wote
wa Mahenge kufuata taratibu zilizopo ili
kila mmoja wao afaidike na rasilimali hiyo.
Naibu Waziri wa
Madini, Doto Biteko (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja baada ya kuzidua
Ofisi ya Madini Wilayani Ulanga katika Mji wa Mahenge uliofanyika tarehe 14
Desemba, 2018. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Mahenge Goodluck Mlinga na
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya.
Naibu Waziri wa Madini,
Doto Biteko (katikati) akikata utepe kuashiria uziduzi wa Ofisi ya Madini
Wilayani Ulanga katika Mji wa Mahenge uliofanyika tarehe 14 Desemba, 2018.
Mbunge
wa Jimbo la Mahenge Goodluck Mlinga akiwahutubia wananchi pamoja na wachimbaji
wadogo wa madini (hawapo pichani) wilayani Ulanga katika mji wa Mahenge, wakati
wa ziara ya Naibu Waziri Biteko.
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akimtambulisha Afisa Mkazi mpya wa
Madini wa Mahenge kwa wananchi (hawapo pichani) baada ya kuzidua Ofisi ya
Madini ya Mahenge tarehe 14 Desemba, 2018.
Wananchi
wa Mahenge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani)
wakati alipofanya mkutano wa hadhara katika mji wa Mahenge wilayani Ulanga.
Wananchi
wa Mahenge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani)
wakati alipofanya mkutano wa hadhara katika mji wa Mahenge wilayani Ulanga.
Kamshina
wa Madini, Dk. Athenes Macheyeki akitia saini katika kitabu cha Afisa Mkazi wa
Madini Mahenge baada ya kuziduliwa kwa Ofisi hiyo tarehe 14 Desemba, 2018.
Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko aliyekaa na Mbunge wa
Jimbo la Mahenge, Goodluck Mlinga kulia.
No comments:
Post a Comment