Na
Greyson Mwase, Morogoro
Maafisa
madini nchini wametakiwa kufuata sheria na kanuni katika utoaji wa leseni za
madini ili kuondoa changamoto ya migogoro kwenye migodi ya madini.
Hayo
yamesemwa leo tarehe 08 Agosti, 2018 na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini,
Profesa Shukrani Manya alipokuwa akitoa mafunzo juu ya taratibu za utoaji wa
leseni za madini kwenye mafunzo ya kazi kwa viongozi na maafisa waandamizi wa
Tume ya Madini yanayoendelea mjini Morogoro.
Alisema
kuwa, ni vyema taratibu za utoaji wa leseni za utafutaji wa madini zikafuatwa ambazo ni
pamoja na mwombaji kubaini eneo linalomfaa kwa utafiti, kujaza fomu ya maombi
na kuwasilisha Tume ya Madini kwa njia ya mtandao na nakala halisi (hard
copies) na ombi kushughulikiwa, kuhakikiwa na kutathiminiwa.
Aliendelea
kueleza taratibu nyingine kuwa ni pamoja
na ombi kupendekezwa na kukubaliwa kupewa leseni, mmiliki wa leseni kuomba
ridhaa kwa mmiliki halali wa ardhi ya kuingia kwenye eneo la utafutaji madini,
mmiliki wa leseni kwa kushirikiana na mamlaka za halmashauri/wilaya kuandaa
mpango wa utoaji wa huduma za jamii.
Akielezea
taratibu za maombi ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini, Profesa Manya
alieleza kuwa ni pamoja na mwombaji kubaini eneo linalomfaa, mwombaji kujaza
fomu ya maombi na kuwasilisha katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi kwa njia ya
mtandao na nakala halisi, ombi kupendekezwa na kukubaliwa kupewa leseni,
mmiliki wa leseni kuomba ridhaa kwa mmiliki halali wa ardhi ya kuingia kwenye
eneo la utafutaji wa madini na mmiliki wa leseni kwa kushirikiana na mamlaka za
halmashauri/wilaya kuandaa mpango wa utoaji wa huduma za jamii.
Katika
hatua nyingine akielezea taratibu za utoaji wa leseni za uchimbaji wa kati na mkubwa Profesa Manya alitaja kuwa
ni pamoja na mwombaji kubaini eneo la
leseni ya utafutaji, kujaza fomu ya maombi na kuwasilisha Tume ya Madini Makao
Makuu kwa njia ya mtandao na nakala halisi (hard copies) na uthibitisho wa
uwepo wa mradi wa uchimbaji, upembuzi yakinifu (feasibility Study) na hati ya
utunzaji wa mazingira.
Alieleza
taratibu nyingine kuwa ni pamoja na ombi kushughulikiwa, kuhakikiwa na
kutathminiwa na ombi kupendekezwa kupewa leseni na kuendelea kufafanua kuwa
hatua nyingine ni pamoja na ombi la leseni kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri
kwa leseni ya uchimbaji mkubwa, (Special Mining Licence), ombi la leseni kukubaliwa kupewa leseni na mmiliki wa leseni
kuomba ridhaa kwa mmiliki halali wa ardhi ya kuingia kwenye eneo la uchimbaji.
“
Mmiliki wa leseni atatakiwa kuomba ridhaa ya uwekezaji kwenye mamlaka ya serikali
za mitaa, mmiliki wa leseni kwa kushirikiana na mamlaka za
halmashauri/wilaya kuandaa mpango wa
utoaji wa huduma kwa jamii” alisisitiza Profesa Manya.
Akizungumzia
kuhusu utoaji wa leseni za uchenjuaji wa madini, Profesa Manya alisema leseni
hutolewa kwa kipindi kisichozidi miaka 10 na Tume ya Madini kwa mtu au
kampuni/ushirika katika eneo ambalo lipo nje ya eneo la mmiliki wa leseni ya
uchimbaji wa madini.
Aidha, akielezea leseni za uyeyushaji wa madini,
Profesa Manya alisema kuwa leseni hutolewa kwa kipindi kisichozidi miaka 25 kwa mtu, kampuni au
ushirika.
Wakati
huo huo akielezea sifa za mwombaji wa leseni, Profesa Manya alieleza kuwa ni
pamoja na mwombaji kuwa na umri usio chini ya miaka 18 na mwenye uwezo wa kifedha, kutokuwa na
makosa katika umiliki wa leseni ya madini iliyo hai au iliyoisha muda au
iliyofutwa ambayo hayakurekebishwa, kutokuwa na makosa yoyote likiwamo la
kutokuwa mwaminifu na kampuni husika kuwa na anwani ya posta na ofisi.
Sehemu
ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (hayupo pichani).
|
Sehemu
ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (hayupo pichani).
|
Sehemu
ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (hayupo pichani).
|
No comments:
Post a Comment